Na Hamisi Kibari
Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki na kiongozi toka China |
Uhusiano wa China na Afrika na China ulianza kwa nchi za Afrika Magharibi za Morocco , Algeria , Suddan, Misri na Somalia .
Lakini zama hizi, uhusiano wa Afrika na China umelenga katika uchumi zaidi ambapo kila mwaka uwekezaji wa China katika bara la Afrika umekuwa ukiongezeka siku hadi siku na kuwa tishio kwa nchi za Ulaya na Marekani.
Inawekeza wapi?
Maeneo makuu ambayo China inawekeza ni kwenye mafuta, gesi na madini, lakini pia imekuwa ikiwekeza katika ujenzi wa barabara na majengo barani Afrika. Imenza pia kujiingiza katika ujenzi wa viwanda barani humo.
Je, wengi wanaukubali uwekezaji wa China
Kumekuwapo na mtazamo tofauti kuhusu uwekezaji wa China barani Afrika. Wapo wanaoamini kwamba uwekezaji huu unaleta maendeleo barani humo kwa vile Wanaingiza pesa, wanatengeneza ajira, kukuza uchumi na ujenzi wa barabara na nyumba.
Pia kwa kulinganisha na mataifa ya magharibi na Marekani, imekuwa ikidaiwa kwamba uwekezaji wa China barani Afrika ni wa kindugu zaidi, ukiwa hauna masharti makubwa kulinganisha na uwekezaji wa nchi za Ulaya na Marekani.
Lakini wapo wanaoamini kwamba uwekezaji wa China barani Afrika ni wa kinyonyaji, kwa maana ya kwamba taifa hilo linalopuiga hatua kubwa kiuchumi na kutishia mataifa mengine kama Marekani limejipanga kunyonya raslimali za Afrika, kadri inavyowezekana sambamba na kuwa soko la bidhaa zao, baadhi zikiwa ni feki kulinganisha na zinazotoka Ulaya.
Kadhalika kumekuwa na hofu ya Wachinga kupunguzia idadi yao katika bara la Afrika. Hii inatokana na baadhi ya Wachina wanaokuja Afrika kujiingiza katika biashara ndogo ndogo ambazo si za kitalaamu kama vile za kuuza mapambo, vinywaji na vitu vidogo vidogo.
Nchini Tanzania , kwa mfano, na hususan katika eneo la biashara la Kariakoo, kumekuwepo na malalamiko kuhusu wingi wa Wachina Tanzania wakifanya shughuli ndogondogo ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania.
Kwa wananchi wa kawaida wanaweza wasilalamike sana kuhusu uwekezaji wao lakini kinachowakera wengi ni bidhaa zao zinazoaminika kuwa na kiwango dunia, vitu kama simu, vifaa vya umeme na kadhalika.
No comments:
Post a Comment